Wakazi wa Barabara ya Iloganzala Jijini
Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti aina ya mwembe kutoa sauti
kama binadamu ukipinga using'olewe.
Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la
kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia
mti kuongea kama binadamu.
Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya
mwembe leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe
huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi
wakishuhudia tukio hilo la ajabu.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka wananchi wa
eneo hilo wanasema jirani na mti huo kuna nyumba iliwahi iligoma
kubomolewa wakati wa upanuzi wa barabara