TAMWA YAJIVUNIA KUWAWEZESHA KIMAFUNZO ZAIDI YA WANAHABARI 2,000.
Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda
Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua moja ya semina za
mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani
ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
KILA
ifikapo Mei 3 ya kila mwaka wanahabari na wadau wa vyombo vya habari
ulimwenguni huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Maadhimisho ya mwaka huu (2017) kitaifa nchini Tanzania yalifanyika
mkoani Mwanza na kushirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa
vyombo vya habari.
Miongoni mwa
hoja zilizoteka mijadala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo
vya Habari Duniani kwa mwaka 2017 jijini Mwanza ni suala zima la usalama
wa wanahabari wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao pamoja na uwepo wa
mafunzo anuai ya mara kwa mara kwa wanahabari kuwanoa zaidi.
Chama cha
Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), ni miongoni mwa taasisi wadau
waliofanikisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani
mwaka 2017 kitaifa yaliofanyika mkoani Mwanza. Bi. Valerie Msoka ni
Mwanachama wa TAMWA, akizungumza katika maadhimisho ya mwaka huu
kuwasilisha ujumbe wa chama hicho kwa wadau wa habari.
Anasema TAMWA
imejitahidi katika kuwanoa wanahabari ili kuhakikisha wanabobea kwenye
maeneo mbalimbali ya uandishi wa habari huku lengo likiwa kuwajengea
uwezo zaidi. Bi. Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
TAMWA hapo nyuma kabla ya uongoziwa wa Mkurugenzi wa sasa wa chama
hicho, Edda Sanga anabainisha wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia
weledi na ubobezi wa wanahabari hasa katika uandishi wa habari za
ukatili kwa jamii.
Anasema tamwa
katika mpango mkakati wake wa kuelimisha jamii kuondokana na vitendo vya
ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kwa kipindi cha mwaka
2015 na 2016 imeelimisha idadi kubwa ya wanahabari kwenye ubobezi wa
uandishi wa habari za ukatili wa kijinsia eneo ambalo limekuwa
likionekana kupwaya kiuandishi.
Wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini zaidi ya wanahabari 2350 na
wahariri 120 walijengewa uwezo wa jinsia ya kuandika habari za ukatili
wa kijinsia zenye kuleta mabadiliko katika jamii ambapo kwa sasa vitendo
hivyo vinatolewa taarifa kwa usahihi ukilinganisha na awali.
Anasema
waandishi hao baada ya kupata mafunzo hayo wamekuwa wakitumia ujuzi huo
kuandika na kuibua habari za vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo
ambalo limesaidia baadhi ya maeneo mamlaka husika kuchukua hatua juu ya
vitendo hivyo, hali ambayo imekuwa ikisaidia kupungua kiasi fulani kwa
vitendo hivyo kwenye jamii ukilinganisha na hapo awali.
Baadhi
ya wanahabari wapiga picha ambao walishiriki mafunzo ya upigaji picha
za ukatili yaliyoandaliwa na TAMWA wakimsikiliza mkufunzi wa mafunzo
hayo, Mwanzo L. Millinga (wa kwanza kulia) kutoka ‘Practical School of
Journalism’ (PSJ) Mratibu
wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kulia)
akizungumza katika moja ya mikutano ya mafunzo kwa wanahabari na wadau
mbalimbali wa TAMWA.
Aidha Bi. Msoka
anaongeza kuwa utaratibu huo wa kuwajengea uwezo wanahabari umekuwa
ukifanywa mikoa mbalimbali huku ukijumuisha wanahabari kuandaliwa
kimafunzo katika semina kadhaa na baadaye kufuatiliwa kwenye utendaji
ili kubaini mabadiliko kimafanikio kabla ya mafunzo na baada ya mafunzo
waliyopata.
Wananchi kwa
upande mmoja nao wamekuwa wakihamasika na kutumia vyombo vya habari
katika kuibua matukio hayo ya kikatili, jambo ambalo limeanza kuleta
mafanikio kiasi fulani.
Bi.Msoka
anaendelea kubainisha kuwa TAMWA katika kutekeleza mradi wake wa GEWE II
kimeweza kuunda kamati za kuelimisha jamii jinsi ya kushughulikia
vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya kumi za Tanzania Bara na
Tanzania Visiwani, ambazo zinawahusisha wanahabari ili kuwezesha jamii
kushirikiana na vyombo vya habari kuweza kuvitolea taarifa vitendo hivyo
bila woga.
Anaeleza kuwa kwa kisi kikubwa kamati hizo zimesaidia kuibua matukio hayo kwa kiasi kikubwa kwa vyombo vya habari.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome
Kitomari akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Hii ni pamoja kujitahidi wanatasnia hiyo kuibua mambo yanayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo ili yafanyiwe kazi, pia kujiepusha na habari ambazo kwa sehemu zinaweza kuleta machafuko na kuhatarisha maisha yao wenyewe au wananchi katika taifa la Tanzania. Kama hiyo haitoshi TAMWA, imeendelea kuwanoa wanahabari katika nyanja nyingine za kimafunzo.
TAMWA ilijiunga katika mapambano ya ajali za barabarani kwa kutoa mafunzo kwa wanahabari mbalimbali. Katika ufafanuzi juu ya hatua hiyo inabainisha kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi.Edda Sanga anasema katika moja ya mafunzo kwa wanahbari kuwa wana kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa.
Anasema licha
ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi
hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa kuwa
wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia.
Sehemu ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wakiwa katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam. Sehemu
ya wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa
katika moja ya mikutano ya mafunzo ulioandaliwa na Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake (TAMWA) jijini Dar es Salaam.