TAMBWE ASEMA ANA UHAKIKA MFUNGAJI BORA ANATOKEA JANGWANI
Amissi
Tambwe wa Yanga amesema kwa jinsi mambo yanavyokwenda, ana uhakika
asilimia 100 mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara atatokea katika timu yake.
Tambwe
amesema anapata nguvu ya kutoa kauli hiyo kutokana na ukweli kwamba,
katika kikosi chao ndipo wanapotokea wachezaji wengi wanaojua kufunga.
Simon Msuva wa Yanga ana mabao 13 akifuatiwa na straika wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa mwenye mabao 12.
Obrey Chirwa wa Yanga, Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar) na Shiza Kichuya wa Simba wote wana mabao 11 na Tambwe mwenyewe anayo kumi.
Tambwe
amesema kwa aina ya uchezaji ya Yanga hadi sasa unaifanya safu yao ya
ushambuliaji kuwa tishio kutokana na kila mmoja kumtengenezea mwenzake
nafasi ya kufunga pale anapopata nafasi.
Tambwe
alisema, kwenye tano bora ya wafungaji katika orodha ya wafungaji
inatawaliwa na wachezaji wa Yanga ambao wamefunga idadi kubwa ya mabao.
Aliongeza
kuwa, katika kufanikisha hilo wanamtoa mfungaji bora, wamepanga kucheza
mechi zote zilizobakia kwa ushirikiano bila ya kunyimana pasi kwenye
safu yao ya ushambuliaji.
“Hadi
hivi sasa ni uhakika kuwa mfungaji bora wa msimu huu anatoka Yanga,
hili halina ubishi na wala halihitaji kubishana na mtu, kikubwa kama
kuna ambaye anaweza kubisha asuburie hadi mwisho aone.
“Pia
tuna michezo mingi kuliko timu nyingine, hivyo nafasi ya kuchukua
ufungaji bora ipo kwetu kwa sababu nyingi,” alisema Tambwe.