Kocha
wa timu ya taifa vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime
amesema watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya Mali katika mchezo wao
wa kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa keshokutwa
Jumatatu kwenye Uwanja wa Port Gentil, Gabon.
Serengeti
imepangwa Kundi B sambamba na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali,
Niger na Angola na inahitaji kushinda michezo miwili ili iweze kufuzu
katika fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika mwaka huu
nchini India.
Akizungumza
kutoka Gabon, Shime alisema kikosi chake kipo tayari kuingia vitani
katika michuano hiyo kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya hivyo
ana imani kubwa watashinda mchezo huo.
“Tunashukuru
kila kitu kinaenda vizuri hakuna mchezaji yeyote majeruhi
tunachosubiria ni kuanza kwa michuano, naamini mechi saba tulizocheza za
kirafiki zimetoa mwanga mkubwa kwa uelekeo wa timu yetu katika michuano
hii.
“Hatuwezi
kuwahofia Mali kwa sababu moja kati ya timu ambazo zinatajwa kuwa ni
ngumu Serengeti Boys ipo, kikubwa ambacho tumekifanya ni kuwaondoa woga
vijana wetu.
“Tumewaongezea
hali ya kujiamini kwa sababu hii ndiyo michuano tuliyokuwa tunaipigania
kupata nafasi, naamini kwamba Mali tutawafunga kikubwa Watanzania
waendelee kutuombea,” alisema Shime.
MECHI ZA SERENGETI
Jumatatu Mali v Serengeti
Mei 18, Serengeti v Angola
Mei 21, Serengeti v Niger