TAMBWE AONDOKA ALIPO KICHUYA, NI BAADA YA BAO DHIDI YA PRISONS
Mshambuliaji
wa Yanga, Amissi Tambwe, amemfunika kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza
Kichuya kwa kukaa muda mrefu bila ya kufunga bao kwenye michezo ya Ligi
Kuu Bara.
Tambwe
mwenye mabao kumi kwenye orodha ya wafungaji msimu huu, juzi Jumamosi
alifunga bao dhidi ya Prisons zikiwa zimepita takribani siku 129 bila ya
kufunga kwenye Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kabla
ya bao hilo la juzi, mara ya mwisho Tambwe kufunga bao kwenye ligi
ilikuwa ni Desemba 28, mwaka jana dhidi ya Ndanda katika ushindi
walioupata Yanga wa mabao 4-0. Mchezo huo pia ulipigwa katika Uwanja wa
Taifa.
Huku
Tambwe akikaa muda huo bila ya kufunga, awali Kichuya mwenye mabao 11,
aliweza kukaa kwa takriban siku 115 akisaka bao katika ligi kuu na kuja
kufanikiwa kufunga dhidi ya Yanga kwenye ushindi wa timu yake wa mabao
2-1, Februari 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Kichuya
kabla ya bao hilo dhidi ya Yanga, mara ya mwisho kwake kufunga bao
ilikuwa ni Novemba 2, mwaka jana wakati timu yake ilipoibuka na ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
“Majeraha
ndiyo yaliyokuwa yakinifanya nisicheze kwa kiwango changu na kushindwa
kufunga mabao, lakini namshukuru Mungu nimerejea kuendelea kuipigania
timu yangu,” alisema Tambwe.
Kwa
upande wa Kichuya, alisema: “Kufunga mabao inakuja tu na wala huwezi
kupanga, ninapopata nafasi huwa nafunga, lakini kikubwa napenda kuona
naisaidia zaidi timu yangu kupata matokeo mazuri bila ya kujali kama
nimefunga au la.”
SOURCE: CHAMPIONI