TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Ndugu waandishi nimewaita leo kutokana na tukio la jana watu
waliojitambulisha kama wananchi wa tarime walienda dodoma kuonana na
waziri wa tamisemi mh simbachawene wakiwa na madai kuwa halmashauri
inakwamisha mradi wa miwa nahuku wao yani wananchi wako tayari kupokea
mradi.
Nianzie hapo ni wapi tumezuia mradi wa miwa kama halmashauri !
Tumehudhuria kikao cha t.i.c Tanzania investment center
ambao wana dhamana ya uwekezaji Tanzania kwa mujibu wa investment act
1997, tarehe 26/04/2017 na kuna makubaliano ya msingi tuliyoingia
Maamuzi ya vikao vya halmashauri vinafanywa na madiwani wa
sehemu husika sio mashirika ya watu walio nje ya eneo husika mfano
madiwani wa tarime-mjini wanahusikaje kwenye mradi kama walivyoonekana
kwenye tv kama mh komote,mh masubo na wengine ilhali siyo halmashauri
yao ?
Baraza la madiwani la tarehe 04/05/2017 limefanya maamuzi
kuwa liandaliwe baraza maalumu kujadili ajenda ya mradi wa miwa
substancial kama tulivyo kubaliana Dodoma na T.I.C na rc,na dc na
madiwani na mbunge.
UTARATIBU WA KUFUATA.
Sisi kama baraza la madiwani wa halmashauri ya
tarime-vijijini tutasimamia utaratibu wa uwazi wa kusimamia kazi ya
mradi wa miwa kupitia vikao kama tulivyoelekezwa na mkurugenzi wa kituo
cha uwekezaji kwa barua yenye kumbukumbu namba ticc/b.10/17/108
Mwekaezaji aje kwenye baraza na pia asitumie nguvu za fedha
kugharamia safari za mara kwa mara zisizo kuwa na dhamira za
kufanikiwa.
Kama mazimio ya kikao cha uongozi wa kituo cha uwekezaji
Tanzania t.i.c pamoja na wadau wa uwekezaji mkoa wa mara ulivyoamua
tarehe 28/4/1017 hilo ndilo tutakalo fuata sio kuanzisha malumbano
yasiyo ya kuanzisha maswala ya kiitikadi na kuchafua watu wa tarime.
SAFARI YA DODOMA.
Safari hiyo iliyosababisha taharuki kwa sababu zifuatazo.
Walio kwenda Dodoma si wananchi ni kikundi cha watu walioandaliwa na wa chama cha mapinduzi ccm.
Hakuna mkutano mkuu wa kijiji chochote kinachoguswa na mradi kilichoteuliwa na kwenda dodoma kwa niaba ya wananchi.
Safari iliandaliwa na mawakala wa mwekezaji na usafiri alitoa ndugu peter zachalia k.n.y kwa nini atumie nguvu zote hizi?
UKWELI KUHUSU UDHALILISHAJI KWA WATU WA TARIME KUHUSU BANGI.
Watu wa tarime wamesikitishwa sana na kauli zinazotolewa za kuwachafua kuwa ni wakulima wa bangi.
Mradi wa miwa unagusa eneo la ukubwa wa ekali (11,000)
katika zote hizo ni ngapi mpaka sasa zinalima bangi? Na katika hao
madiwanai wa ccm walioenda Dodoma nani ana bangi katika kata yake?
Kwa sababu hiyo huu ni uchafuzi tu sisi tarime ndio tunaolima ndizi,mahindi,mhogo,alizeti,mtama
na viazi na tunalisha mikoa ya kanda ya ziwa kwani tuna misimu ya mvua
miwili hili liko wazi na moja ya mapato yetu hapa halmashauri ni ushuru
wa mazao unatupatia zaidi ya milioni mia tatu kwa mwaka wa fedha .
RAI.
Waziri alipaswa kuwasiliana na mimi kama mwenyekiti wa
council kupata mwelekeo wa nini kinaendelea na sio kutoa maamuzi ya
upande wa mwekezaji bila kusikiliza madiwani kwa maana ya halmashauri
au angekuja kwa dharura tarime akae na sisi kuliko kuweka taharuki
nahuku tayari tulikuwa tumekwisha kaa vikao na T.I.C
HAYA NDIYO MAAZIMIO YA KIKAO CHA UONGOZI WA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA T.I.C PAMOJA NA WADAU WA UWEKEZAJI MKOA WA MARA.
Rejea na somo tajwa hapo juu.
Napenda kukushuru sana kwa kuweza kuhudhuria kikao cha
uongozi wa kituo cha uwekezaji pamoja na wadau wa uwekezaji katika mkoa
wa mara kilichofanyika Dodoma tarehe 26/4/2017 kwenye ofisi za tic
zilizopo katika jengo la lapf.uwepo wako katika kikao hiki ni wa muhimu
sana na ulichangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia maazimio chanya
yanayohusu uwekezaji wa kiwanda cha sukari unaotarajiwa kufanyika katika
wilaya ya tarime.
Yafuatayo ni maazimio ya kikao cha uongozi wa kituo cha
uwekezaji pamoja na wadau wa uwekezaji katika mkoa wa mara yaliyofikiwa
baada ya majadiliano yaliyoshirikisha wataalamu na wadau wa ngazi zote
katika wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kituo cha uwekezaji
halmashauri ya wilaya ya tarime halmashauri za vijiji pamoja na ofisi
ya mkuu wa mkoa wa mara,na mh mbunge wa tarime vijijini na ofisi ya mkuu
wa wilaya ya Tarime.
1.Mkurugenzi wa halmashauri aandae taarifa inayohusu mradi
wa kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari (kwa maandishi) na
kuwasilisha kwenye baraza la madiwani ili mradi huo uweze kujadiliwa.
2.Zoezi zima la upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji ni vyema likafuata utaratibu,uwazi na ushirikishwaji.
3.Viongozi wote ni bora wakaacha kuzunguma mambo ya kutisha
na kujitahidi kuzungumza maneno mazuri yanayohusu mkoa wa mara na
wilaya ya tarime ili kuweza kuwavutia wawekezaji wawekeze zaidi katika
mkoa huo na maeneo mengine.
4.Taratibu zote zilizoachwa bila kutekelezwa katika zoezi la upatikanaji wa ardhi ni vema zikafuatwa.
5.Viongozi wote(wawakilishi wa wananchi)wahakikishe vijiji vyote wanaozungukwa na mradi huu vinanufaika na mradi.
6.Mkuu wa wilaya na mbunge washirikiane kumaliza migogoro
midogo iliyopo ili kuweza kuweka nguvu za pamoja na kuhamasisha
uwekezaji.
7.Viongozi waache kutumia vyombo vya habari kama mazungumzo yanayoendelea baina yao hayajafikia muafaka.
8.Hatua zote za kuhaulisha ardhi katika ngazi ya halmashauri zifanyike haraka na kwa ushirikishaji wa wadau wote muhimu.
9.Tusonge mbele kwa pamoja katika kuharakisha na kufanikisha uwekezaji huu muhimu.
10.Eneo la kiwanda na maeneo ya mashamba yatakayotumika kwa
ajili ya uwekezaji yapewe kipaumbele stahiki ili tuharakishe uwekezaji
huu muhimu.
11.Sisi sote sasa twende mbele kwa ajili ya kuunga mkono na kufanikisha uwekezaji huu kwa haraka
Pamoja na maazimio haya nimeambatanisha pia na taarifa ya
kikao ili kuweza kujikumbusha mambo mbalimbali tuliyojadili katika
kikao, hayo ndiyo makubaliano yaliyojadiliwa na tunasubiri yakafanyiwe
kazi.
Asanteni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini,
Moses Msiwa Yomami
|