TAMBWE ANASEMA YUKO FITI KABISA NA KIPANGWA LEO, PRISONS WAMEONDOKA
Mshambulizi
Mrundi, Amissi Tambwe yupo fiti na amesema akipata nafasi kwenye kikosi
cha kwanza cha Yanga dhidi ya Prisons, basi atahakikisha ni lazima
afunge bao.
Yanga
leo Jumamosi inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho
maarufu kama Kombe la FA kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa
muda mrefu, Tambwe raia wa Burundi alikuwa nje ya uwanja akisumbuliwa
na majeraha ya goti, sasa amepona na amesema: “Nikipangwa kesho (leo),
nitapambana nifunge japo bao moja.”
Tambwe alisema ana hamu ya kuzifumania nyavu kwani ni muda mrefu amekaa bila ya kufunga bao lolote jambo linalomuumiza moyoni.
“Namshukuru
Mungu nipo fiti baada ya kupona goti lililonisumbua kwa muda mrefu,
endapo nitapata nafasi ya kucheza mechi ya kesho (leo), nitahakikisha
napambana vilivyo ili niweze kufunga nitulize roho yangu,” alisema
Tambwe.