MSUVA SASA APEWA MAZOEZI YA KUPIGA KONA ZA KUMALIZA KAZI
Yanga
jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na muda
mwingi winga Simon Msuva alionekana akipewa mazoezi ya kupiga kona
zinazoelekea moja kwa moja wavuni.
Shiza
Kichuya wa Simba, amewahi kuifunga Yanga bao la kona ya moja kwa moja
Oktoba mwaka jana, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha timu
hizo uwanjani hapo na kutoka sare ya bao 1-1.
Kocha
Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi katika mazoezi hayo alionekana akimnoa
Msuva kupiga kona hizo zinazoelekea nyavuni zenyewe ikionekana ni
maandalizi ya mechi ya leo dhidi ya Prisons.
Yanga
inacheza na Prisons mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho
maarufu kama Kombe la FA, leo kwenye Uwanja wa Taifa na mshindi
ataungana na Simba, Azam FC na Mbao FC katika nusu fainali.
Wakati
Mwambusi akitoa maelekezo yake kwa Msuva kuhusu upigaji huo wa kona,
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina alikuwa akifuatilia kwa umakini
zoezi hilo.
Baada
ya kumaliza mazoezi hayo, Mwambusi amesema kuwa; “Haya ni mazoezi ya
kawaida tu kwa Msuva, tuna mechi nyingi muhimu mbele hii ni moja ya
mbinu za ushindi.”
SOURCE: CHAMPIONI