SAMATTA ANAVYOONEKANA KATIKA UZI WA YANGA, NI ZAWADI KUTOKA KWA MSUVA
Hatimaye mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mbwana Samatta kwa mara ya kwanza ameonekana akiwa na uzi wa Yanga.
Samatta ambaye alisajiliwa na TP Mazembe
ya DR Congo alikopata mafanikio makubwa akitokea Simba, ametupia picha
ya jezi ya Yanga, namba 27 inayovaliwa na Simon Msuva.
Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji
amemshukuru Msuva kwa kumtumia zawadi ya jezi hiyo na kuitupia hali
inayomfanya aonekane “mpya”.