Picha: MKUU WA MKOA WA PWANI MHANDISI NDIKIRI AISHUKURU TANESCO KWA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikiri, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meenja Uhusiano wa Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa
vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha
Aprili 29, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikiro, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi
kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.
Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo
yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za
kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.
"Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri
sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu
ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa
njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi." Alisema.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO kama mtoa
huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake
wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha
mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi."
Alisema.
Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa
vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma
kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. "Tumeungana nanyi leo
Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo
chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina
hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali
yawe safi." alisema
Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro,
aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa
TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la
kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya
kituo hicho cha afya.
Mhandisi Ndikiro, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake
Bi leila Muhaji, (katikati), akitoa
hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro,
na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga
Wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani
Mhandisi Ndikiro akimshukuru Bi.Nisile, huku Bi. Leila (wapili kushoto) na Bi Salama Juma, ambaye ni Afisa Uhusiano TANESCO
Wafanyakazi hawa wa TANESCO wakiwa wamebeba sehemu ya vifaa hivyo
Mhandisi Ndikiro, (kulia) na Bi. Leila Muhaji wakifyeka majani kwenye eneo la Kituo hicho cha Afya
Wafanyakazi wa TANESCO wakifagia mazingira kuzunguka kituo hicho
Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akifafanua baadhio ya mambo kwa waandishi wa habari
Watumishi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha, wakifyeka nyasi
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Mhandisi Ndikiro akiwa amenyanyua baadhi ya vifaa alivyokabidhiwa
Watumishi wa kituo hicho cha afya wakikusanya sehemu ya vifaa hivyo
Mtumishi wa kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, akwia amebeba sehemu ya vifaa hivyo















