OMOG ALIVYOSHANGAZWA NA VIJANA WAKE KUIPASUA MBAO DAKIKA 7 ZA MWISHO
Kocha
wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, ameweka wazi kwamba kitendo cha
wachezaji wake kushinda mechi dhidi ya Mbao kilimshangaza hata yeye
kutokana na kuamini mechi hiyo ingeisha kwa sare au kupoteza.
Omog
kwa mara ya kwanza alivunja mwiko wa Simba kushinda Uwanja wa Kirumba
baada ya kupita miaka saba mfululizo bila, walipopata ushindi mbele ya
Mbao kwa mabao 3-2.
Kocha
huyo amesema kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa mechi ngumu ambazo amewahi
kukutana nazo akifundisha soka kwani huwa ngumu kwa timu ambayo
imefungwa mabao mawili kuweza kupindua matokeo.
“Sikuwa
na imani kubwa ya kushinda baada ya kufungwa yale mabao mawili japo
nilitambua tuna nafasi ya kushinda kwa sababu sisi tuna uzoefu zaidi ya
wapinzani wetu ambao walikuja kuchoka katika dakika za mwisho na sisi
ndiyo tukapata mabao yetu.
“Ila
niwapongeze Mbao kwa ushindani ambao wametuonyesha na niseme hii ni
moja ya mechi ngumu ambazo nimekutana nazo kwenye maisha yangu ya soka
kwani kutoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda siyo jambo dogo hata
kidogo.
“Sasa
tumekaa kwenye uongozi wa ligi na niseme kwamba hiki tulichokifanya
mbele ya Mbao ndiyo tutakifanya kwenye mechi nyingine zijazo ikiwemo
mchezo wetu dhidi ya Toto,” alisema Omog.