AMISSI TAMBWE ANAO TU SIMBA, UJUMBE WAKE MWINGINE KWAO, HUU HAPA
Baada
ya kupona kwa mastraika wa Yanga, Donald Ngoma na kiungo Thabani
Kamusoko, straika raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ameibuka na kusema
wapinzani wao Simba wasitarajie Yanga itapoteza mchezo wowote tena hadi
wanachukua ubingwa.
Ngoma
na Tambwe kwa nyakati tofauti walikuwa nje ya kikosi hicho kutokana na
kusumbuliwa na majeraha ya goti lakini kwa sasa wamepona na Jumamosi
iliyopita Ngoma na Kamusoko, walidhihirisha hilo kwa kucheza katika
mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria.
Tambwe
amesema kuwa uwepo wa nyota hao utawafanya wazidi kupambana na Simba
kwenye mbio za ubingwa na hatimaye kuwapiku na kuwa mabingwa hata kwa
tofauti ya mabao kama watalingana pointi.
Tambwe
amesema tangu amewaona Kamusoko na Ngoma wameanza kucheza wikiendi
iliyopita, hakika amepata nguvu ya kufanya vizuri zaidi ya hapo na
kwamba kama hakitatokea kikwazo kingine basi Simba wao wajaribu
kuelekeza nguvu mahali pengine tu kwani suala la ubingwa litakuwa gumu
sana kwao.
“Najua
wenzetu wapo mbele kwa tofauti ya pointi mbili baada ya kuifunga Mbao
FC, juzi lakini naomba wajue tu kuwa kupona kwa Ngoma na mimi huku
Kamusoko naye akiwa fiti, hii ni chachu kubwa ndani ya safu yetu ya
ushambuliaji ambayo utaona kila mmoja atakuwa amepata nafasi kubwa ya
kucheza na kufunga kwani sisi kila mmoja ana uwezo wa kumtafutia
mwenzake na kufunga mwenyewe.
“Simba
wasitegemee ubingwa kama sisi tupo hata kama wamekuwa na kasi nzuri,
lakini wajue kuwa tutapambana hadi mwisho,” alisema Tambwe.
SOURCE: CHAMPIONI