MRADI WA ECOPRC WAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI JUU YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU NA MABADILIKO YA TABIA NCHI, MJINI MOROGORO.
Mratibu wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi
shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw.
Elinasi Monga akifundisha somo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo
aliweza kukazia suala la waandishi wa habari kujua visababishi na
viashiria ambavyo ni vyema kujua na kuweza kuvifanyia kazi kwa ufasaha
zaidi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Picha
zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.
Katika mafunzo hayo Mratibu wa Mradi huo alisema kuwa wakulima wadogo
wadogo ndiyo wanaathika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa
wamekuwa hawana uelewa mzuri katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliongeza jambo lingine linalorudisha nyuma ni serikali za mitaa kukosa
mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwisho alisisitiza uongozi mbovu katika sekta ya misitu huchangia
uharibifu wa misitu kwa kiasi kikubwa.
`
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Elinasi Monga akisisitiza jambo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akifundisha somo juu ya
kiwango vya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, Nyenzo shirikishi pamoja
na umuhimu wa misitu ya jamii ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari
kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017
mjini Morogoro.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhiria mafunzo hayo.
Kikundi cha tatu kikijadiliana.
Kikundi cha pili kikijadiliana.
Kikundi cha kwanza wakijadiliana.
Kuhusu Mradi wa ECOPRC
Mnamo tarehe 25 Oktoba 2012, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Ufalme wa Norway zilikubaliana kuingia katika mkataba wa utekelezaji
wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wananchi kupitia Mafunzo ya Usimamizi
Shirikishi wa Misitu (USM), Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa
Kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) na Mabadiliko ya
Tabianchi (“Empowering Communities through Training on Participatory
Forest Management, REDD+ and Climate Change Initiatives – ECOPRC”).
Lengo kuu la mradi huu ni kujenga uwezo wa vikundi mbalimbali vya
kijamii ili viweze kusimamia misitu kwa uendelevu na kwa faida; lengo
mahususi ni kuongeza tija katika usimamizi endelevu wa rasilimali za
misitu kwa namna ambayo inaleta faida kijamii, kiuchumi, kimazingira na
kiutawala bora kwa jamii zinazojihusisha na shughuli za Usimamizi
Shirikishi wa Misitu, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi. Mradi huu ni
wa miaka mitano, unaotekelezwa na washirika wanne ambao ni Chuo cha
Misitu Olmotonyi (Mshirika Kiongozi), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa
Misitu Tanzania (MJUMITA); Kituo cha Misitu na Watu (RECOFTC) cha
Bangkok-Thailand na FORCONSULT, kitengo cha ushauri elekezi cha Kitivo
cha Misitu na Hifadhi ya Mazingira Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine.
Shughuli za Mradi zinatekelezwa katika malengo mahususi sita:
1. Programu ya kujenga uwezo wa Taifa katika USM/MKUHUMI umeandaliwa na
kurasimishwa kupitia mafunzo yatokanayo na uzoefu na uwezo wa
kusharadiana na mazingira halisi.
2. Ufanisi na Uwajibikaji wa Halmashauri za Wilaya na Watumishi wake
Unaongezeka Kwa Kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau katika nyanja za
USM, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi.
3. Kuboresha Maarifa na Uelewa wa Viongozi wa Vijiji Katika usimamizi
endelevu wa shughuli za USM, MKUHUMI Mabadiliko ya Tabianchi.
4. Kutoa Fursa kwa Watendaji, Watekelezaji na Watoa Maamuzi ili Waweze
Kupitia, kufanya Mageuzi na Kutambua Mazingira Wezeshi kwa Sera za USM,
MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi.
5. Miundombinu ya Chuo cha Misitu inaboreshwa ili kuongeza ufanisi
katika kutoa Mafunzo bora
6. Usimamizi na Uendeshaji wa Mradi.
Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Daniel Lucas akifundisha somo juu ya
kuimarishwa Utawala Bora katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambavyo
ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo
hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akifunga mafunzo
ya waandishi wa habari yaliyofanyika Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro.
Alisema kuwa nia ya nia ya mradi wa ECOPRC ni kuziwezesha jamii ziishizo
vijijini na wadau wengine kupitia mchakato mahsusi wa kuwajengea uwezo
ili kuboresha Usimamizi Shirikishi wa Misitu na kuwa na uboreshaji wa
njia za maisha katika jamii. lengo la mafunzo haya ni kuhamasisha
serikali katika Usimamaizi Shirikishi wa Misitu ili kuwa na faida za
kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa jamii zinazojihusisha na Usimamizi
Shirikishi wa Misitu. Kushoto ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard
Giliba.
Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Mussa Twangilo (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, James Lyatuu (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Henry Mwakifuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Beatrice Philemon (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Safia Maftah (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Saada Mbarouk (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa Blogger na mwandishi wa habari, Cathbert Angelo Kajuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Josephine Mallango (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Agrey Evarist (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Kalokola Aporinary (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Prosper Kaijage (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya Mradi wa kuwajengea uwezo
jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na
mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC) mjini Morogoro wakiwa katika picha ya
pamoja na wawezeshaji wao.