MABADILIKO VIONGOZI WA UHAMIAJI YAFANYIKA...ANGALIA HAPA MAJINA MAPYA YA VIONGOZI WA MIKOA
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji Nchini Dr. Anna Peter Makakala amefanya mabadiliko
makubwa ya Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja
na kuwateua Wakuu Wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo katika Mikoa
iliyopo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Katika
Mabadiliko haya Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Faustine Nyaki
aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza amehamishiwa mkoa wa Simiyu
wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Selemani Bandiho Kameya amehamishiwa Mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Paulus
Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Manyara Naibu Kamishna Peter Jerome Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma
kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Ali Mohamed ambaye amehamishiwa
kuwa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Arusha.
Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Mkemi Mhina Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Muhsin
Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi na Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Othman Khamis Salum ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi
Unguja.
Katika
mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa Mikoa wamebaki katika
Vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Morogoro Naibu Kamishna wa Uhamiaji Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Lindi Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Laurent Shauri, Mkuu
wa Uhamiaji Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Alexander
Ihano na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Fredrick
Eustace Kiondo.
Wengine
waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Abdallah Ramadhani Towo mkoa wa Kagera na Naibu Kamishna wa
Uhamiaji Anastazia Gasper Ngatunga mkoa wa Shinyanga.
Katika
mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Makakala pia
amewateua Viongozi wa Uhamiaji wa Mikoa wapya katika baadhi ya mikoa
hapa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mary Francis Palmer kuwa
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Plasid Mazengo, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa
Uhamiaji James Andrew Mwanjotile, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope Jaffer Kawawa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Iringa, na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Hosea Alphonce Kagimbo
Mkoa wa Njombe.
Wengine
ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Rashid Salum Magetta Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Songwe, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Carlos John Haule, Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Julieth Deodatus
Sagamiko Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Albert Joseph Rwelamila, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro na
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Laurent Eranga, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Mwanza.
Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Crispin Crispin Ngonyani ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Shaban Omar
Hatibu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Katavi, Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Remigius Ibrahimu Pesambili Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma na Mrakibu
Mwandamizi wa Uhamiaji Novaita Edmund Mrosso ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Mbeya.
Aidha
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa kuwa
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid
Amani Karume [AAKIA] na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji
Fulgence Andrew Mutarasha kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere[JNIA].
Imetolewa na
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini
Dr. A. P. Makakala
3 Machi 2017