BUNGE LAANZA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA



Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu yake.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt Jayaka Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge.


Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa na wabunge wanawake kwenda kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini Dodoma.

Mhe. Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo Bungeni Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika leo Bungeni Mjini Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mama Devotha Gabriel.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa awamu ya pili  saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt Jayaka Mrisho Kikwete akifuatilia shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbusi
Powered by Blogger.