Waziri Nape Aunda Kamati Kwa Ajili Ya Kuchunguza Tukio La kuvamizi kwa Kituo Cha Habari Cha Clouds.
|
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
katika Picha) alipofanya ziara katika Chombo cha Habari cha Clouds leo Jijini
Dar es Salaam.
|
|
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto)
akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Peter
Serukamba(MB).
|
Habari na
Shamimu Nyaki
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya
watu watano itayoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan
Abbas kuchunguza tukio la uvamizi lilofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda katika chombo cha habari cha Clouds Media.
Akiongea
katika ziara aliyoifanya leo Jijini Dar es Salaam katika chombo hicho Mhe.Nape amesema Kamati
hiyo itafanya kazi ndani ya masaa 24 kuanzia sasa huku akiwataja wajumbe
wengine kuwa ni Bw. Frank
Balile,Bibi.Johanes Neng’ida,Bw.Jessy Kwayu na Bibi. Mabel Mabisa kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano Serikalini (TCRA).
“Kamati
hii ipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Bw.Paul Makonda ili tuwe na taarifa iliyokamilika na kujua hatua
itakayofuata” alisema Mhe.Nape
Aidha
Waziri Nape ameeleza kuwa kitendo cha uvamizi kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa
kipo kinyume na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwa kuwa sheria
hiyo ipo kwa ajili ya kulinda wanatasnia hao.
Aliongeza
na kufafanua kuwa Serikali imesikitishwa na kitendo hicho na ndio maaana akaunda
kamati ya uchunguzi itakayokuja na taarifa kamili huku akiwataka wanatasnia ya habari
na wananchi kuwa watulivu na kusubiri majibu ya uchunguzi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Habari ya Clouds Bw.Joseph Kusaga amemshukuru
Waziri Nape kwa kuonyesha ushirikiano na kuwa pamoja katika jambo hilo huku
akifurahishwa na namna Serikali inavyowajali wadau wa Habari.
Kwa
Upande wake Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT)
Bw.Reginald Mengi amempongeza Mhe. Waziri kwa hatua ya kuunda kamati ya
uchunguzi kwakuaanaamini itatoa matokeo
chanya yatakayolinda heshima ya Tasnia ya Habari nchini.
“Uamuzi wa kuunda kamati hii ni jambo la
hekima na busara linaloendana na misingi ya taaluma ya habari nasi tutakuwa
radhi kuunga mkono hatua zitachukuliwa
katika kulinda uhuru wa habari nchini” alisema Bw.Mengi.
Tukio
la kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe Paul Mkonda limetokea usiku wa Machi 17 mwaka huu.