Jumla ya wawezeshaji 432 wa mpango
wa elimu ya msingi kwa walioikosa(Memkwa) wamehitumu mafunzo ya mwezi mmoja
ambayo wamepata kwa ajili ya kufundisha watoto ambao wapo nje ya mfumo wa shule
katika Wilaya nne za Mkoa wa Mara ambazo ni Butiama, Bunda, Tarime na Musoma
Mpango huo unatekelezwa kwa
ushirikiano wa taasisi ya Graca Machel Trust, Mara Alliance na Serikali ya Mkoa
wa Mara na unalenga kuwafikia watoto 20,000 wenye umri wa miaka 7-17.
Mahafali ya wawezeshaji hao yalifanyaika jana katika chuo cha
Mandeleo ya Jamii cha Buhare Mjini Musoma na kuhudhuliwa na wadau wote wanatekeleza mpango huo
wakiwemo viongozi wa serikali.
|