MIEZI MINNE BAADA YA UZINDUZI WA NDEGE MBILI ZA ATCL (BOMBARDIER), WAKUSANYA BILIONI 9
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi
anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa
kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai
kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa.
Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada
ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la
Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo
ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na
kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena
Serikalini kwa asilimia 100.
KUMBUKUMBU:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na
maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi
ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa
ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe
Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye
ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier
Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam
Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.