March 22, 2017 Waziri wa habari,
utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alikabidhiwa ripoti na kamati
aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza tukio la tuhuma za uvamizi alioufanya
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika ofisi za Clouds Media
Group usiku akiwa na Askari wenye silaha.
Waziri Nape baada ya kupokea ripoti
hiyo aliongea na Waandishi wa habari kueleza kuwa hatua inayofuata ni
yeye kuiwasilisha ripoti hiyo katika ngazi kuu ya uongozi akiwemo Rais
Magufuli ili hatua stahiki iweze kuchukuliwa.
Baadhi ya walioonesha kuipokea taarifa
za ripoti hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye
akaamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akipongeza
hatua ya Waziri Nape.