|
Daktari
bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa
aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani,
shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli.
Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na
taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea
kuchukua jukumu la kumsaidia. Mkuu wa Jengo la Sewahaji Bibi. Salome Mayenga
(kushoto) na Mkuu wa Wodi namba 24 Sewahaji, Muhimbili Bibi. Georgina
Kabaitileki.
|
|
Daktari
bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa
aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani,
shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli.
Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na
taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea
kuchukua jukumu la kumsaidia.
|
|
Mkazi
wa mkoa wa Mara ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa mgonjwa kufuatia majeraha ya kuunguzwa
na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi,Bibi. Neema Mwita akimshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo
pichani) kwa kitendo chake cha kumfariji na kumsaidia kupata matibabu ya hayo
wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma.
Picha
na: Frank Shija
|
Na.
Georgina Misama
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa
moyo wake wa kujitoa na kuwajali wanyonge hasa wagonjwa wasiojiweza na wenye
uhitaji wa gharama za matibabu.
Hayo
yamesemwa leo na Bi. Neema Mwita Wambura maarufu kama ‘Mgonjwa wa Magufuli’
wakati alipotembelewa na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili ambako alilazwa kwaajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata
majeraha ya moto.
“Ninamshukuru
sana Mhe. Rais Magufuli kwa msaada wake katika matibabu yangu. Hivi sasa mimi
nina maendeleo makubwa, naweza kuongea, kula na hata kugeuza shingo yangu.
Nitamuombea Rais Magufuli mpaka siku naingia kaburini, Mungu ambariki” anasema
Neema.
Akisimulia
mkasa uliompata Neema anasema kwamba alimwagiwa maji ya moto na mumewe baada ya
kuchuma mahindi mawili (2) shambani bila ya ruhusa yake. Mumewe huyo alitoweka
na ndugu za Neema walihofia kumchukua kwa kuogopa kudaiwa mahali iliyolipwa na
mumewe kama taratibu za kumuoa.
“Hakuna
ndugu yangu hata mmoja aliyejitokeza kunisaidia kipindi chote cha matibabu.
Walihofia kama ningefariki ingempasa huyo ndugu kurudisha mahali ambayo mume
wangu alitoa. Nilikuwa nasaidiwa na majirani tu, nilikata tamaa ya kuishi
nilikuwa nasubiri siku yangu ya kufariki ifike,” anasimulia Neema.
Aidha,
Neema anawashukuru watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela
wakiwemo manesi na madaktari kwa upendo na msaada mkubwa waliompatia toka siku
wanampokea katika hospitali hiyo mpaka sasa ambapo anatarajia kurudi nyumbani.
“Nawashauri
watanzania wasisikilize maneno ya watu wanaolalamika kwamba Muhimbili huduma
sio nzuri, si kweli,kwa muda wote niliokaa hapa nimepatiwa huduma nzuri, tena
kwa upendo na upole”
Akielezea
maendeleo ya afya ya Neema, Mkurugenzi wa Upasuaji ambaye pia ni Daktari bingwa
wa upasuaji Dkt. Ibrahimu Mkoma amesema kwamba, Neema alipokelewa hospitalini
hapo tarehe 06/07/2015 akitokea Mkoa wa Mara wilaya ya Musoma , Neema alikuwa
na majeraha ya mwaka mmoja toka aunguzwe.
Mpaka
sasa Neema ameshafanyiwa oparesheni tatu kwa nyakati tofauti, zilizohusisha
kutengenisha baadhi ya viungo kwani shingo, kifua na mkono wa kushoto
vilishikana. Halkadhalika ilibidi kutoa ngozi ya sehemu ya mwili ili kufunika
sehemu zile zilizoathirika zaidi.
“Ni
katika kipindi hicho cha matibabu, Mhe. Rais alimuona Neema na kuguswa na hali
yake, ambapo aliamua kumsaidia mpaka hivi sasa mnavyomuona. Neema sasa amepona
na ataweza kuihudumia familia yake vizuri”, aliongeza Dkt. Mkoma.
Akiongelea
Moyo wa kujali wanyonge alionao Rais JPM, Dkt. Mkoma anasema kwamba Rais
anaongoza kwa mfano, hivyo watanzania hawana budi kujifunza moyo huo wa kujali
na kusaidia wahitaji wakati wote kwenye jamii.
Aidha,
Dkt. Mkama ametoa wito kwa wadau na taasisi zinazohusika katika kutoa elimu kwa
umma hususan madhara ya vitendo vya kikatili kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia
sehemu zenye ukubwa wa tatizo hilo ili kumaliza kabisa majanga ya aina hiyo.