Maafisa
Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya
Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa
na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.
Rai
hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao
(EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa
tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini
kinachoendelea Mkoani humo.
Dkt.
Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni kuhuisha matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa
taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi
kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana na wakati ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.
“Wakala
kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali kutengeneza
tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha
wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.
Mtendaji
Mkuu huyo ameongeza kuwa tovuti za taasisi zisitumike tu katika kutoa taarifa
za huduma na bidhaa zao bali zitumike kuelezea mambo mengine muhimu
yanayofanywa na taasisi hizo.
Akielezea
kuhusu tovuti kuu ya Serikali, Dkt. Bakari amesema ni muhimu kuhakikisha
taarifa muhimu na za kudumu za taasisi husika zinawekwa ili kusaidia wananchi
kufahamu kiundani kazi wanazozifanya.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano (TAGCO), Bw.Innocent Mungy amesema mbali na kuweka
taarifa katika tovuti za Serikali, ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini kutumia
mitandao ya kijamii kufikisha taarifa muhimu kwa wananchi .
“Kutokana
na maendeleo ya teknolojia duniani hasa katika upande wa mawasiliano, matumizi
ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakileta tija kwa taasisi za Umma kwani yanasaidia
Serikali kujibu haraka hoja zinazowasumbua wananchi”alisema Mungy.
Pia
aliwataka Maafisa Mawasiliano kuwa wabunifu katika kutumia mitandao ya kijamii kwani
mitandao hiyo inatoa fursa ya kushirikiana, kutangaza huduma na bidhaa za
taasisi, kufahamu matatizo ya wananchi