|
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na Maafisa
Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali
kinachofanyika Mkoani Dodoma.
Na
Lorietha Laurence-Dodoma
Maafisa
Mawasiliano Serikalini wametakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kuanzisha mawasiliano ya kimkakati
yatakayosaidia kuhamasisha na
kusukuma agenda muhimu za kitaifa ikiwemo kuelekea uchumi wa viwanda,vita dhidi
ya madawa ya kulevya na uzalendo.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye alipokuwa akifungua mkutano wa 12 wa Maafisa Mawasiliano Serikalini
Mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza kuwa kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya
Serikali na wananchi.
“Maafisa
Mawasiliano ni daraja muhimu katika kutoa taarifa kwa umma na kujenga taswira
ya Serikali ili kufikia malengo yaliyowekwa hivyo basi kwa kufahamu jukumu hili
ni wajibu wa kila Afisa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha umma kuhusu
mkakati wa maendeleo uliowekwa na serikali“alisema Waziri Nape.
Aliongeza kuwa Maafisa Mawasiliano wahakikishe baada ya
kikao kazi hicho wanatoka na mpango mzuri wa mawasiliano ya kimkakati ili
kurahisisha utoaji na upatikanaji wa habari na taarifa muhimu kwa wananchi
utakawasaidia kujua mpango wa maendeleo na utekelezaji wake.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Elizabeth Simon Kitundu
ameishukuru Wizara kuandaa mafunzo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini na
kuyafanyia Mkoani Dodoma kwani kwa kufanya hivyo itarahishisha mfumo wa
kimawasiliano na kutangaza fursa zilizopo Mkoani humo.
“Mmekuja
kpindi kizuri sana ambapo tayari
serikali imeashaanza kuhamishia
Wizara na Taasisi zake katika mkoa wetu ukizingatia Mji wa Dodoma una fursa nyingi za uwekezaji, na tayari huduma muhimu
za msingi kama vile barabara,hospitali,huduma za maji,makazi na shule zinazidi
kuimarishwa “ alisema Bibi. Elizabeth.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw.Innocent
Mungy aliahaidi kuufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Nape ili
kuhakikisha wanaisemea Serikali.
|