Waziri Mkuu Apokea Wanachama Wapya 89 Kutoka kutoka CUF, CHADEMA na ACT .....Yumo aliyekuwa Katibu Mwenezi wa kata wa CHADEMA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama saba kutoka vyama vitatu vya
upinzani ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) na wengine 82
kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walikuwa wapiga debe.
Wanachama
hao wamepokelewa jana mchana (Ijumaa, Mei 25, 2018) wakati akizungumza
na wananchi mara baada ya kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa
katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani
Lindi.
Waziri
Mkuu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alipokea kadi nne za
CUF, moja ya ACT na mbili za CHADEMA kutoka kwa wanachama hao saba kabla
hajawakabidhi kadi za CCM. Wanachama hao saba waliokabidhiwa kadi mpya
za CCM pamoja na wenzao 82, walikula kiapo cha uaminifu mbele ya Waziri
Mkuu.
Shangwe
zililipuka uwanjani hapo wakati aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA
kata ya Nachingwea, Bw. Ismail Hamisi alipokabidhi kadi yake kwa Waziri
Mkuu.
Akisoma
risala kwa niaba ya wanachama wenzake walioamua kujiunga na CCM, mkazi
wa Ruangwa mjini, Bw. Fred Mnimbo alisema wameamua kurudi kwa sababu
yale waliyotarajia yafanyike upinzani hayaonekani.
“Tumegundua
upinzani wa sasa ni maslahi binafsi na si wa kuwatumikia wananchi;
kinachosemwa sicho kinachotendwa na wapinzani na pia tumeamua kuunga
mkono juhudi anazofanya Rais John Pombe Magufuli,” alisema Bw. Mnimbo
katika risala hiyo.
Alisema
wameamua kuhamia CCM kwa sababu Serikali iliyopo madarakani kwa sasa
inatekeleza mahitaji ya Watanzania kwa asilimia 90 na pia wanataka
kumuunga mkono mbunge wao wakiwa katika chombo kimoja ili waijenge
vizuri Ruangwa na Tanzania kwa ujumla.
“Tunataka
kuunga mkono usimamizi mzuri wa rasilmali zetu hasa mazao ya korosho na
ufuta kutokana na jinsi unavyoyasimamia kikamilifu hasa mikoa ya
Kusini. Kaulimbiu ya Ruangwa kwa maendeleo inawezekana, imedhihirika kwa
vitendo kwa sababu kila mmoja anaona kwamba Ruangwa ya jana si Ruangwa
ya leo, maendeleo yanaonekana kwa mafanikio makubwa,” alisema huku
akishangiliwa.
Akitoa
utambulisho wa wanachama hao wapya, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw.
Barnabas Essau alisema wanachama hao wameamua kujiunga na CCM kwa sababu
wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano.
Novemba
5, mwaka jana, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vya CUF
na CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera,
wilayani Ruangwa. Pia Desemba 29, 2017, alipokea wanachama 60 kutoka CUF
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nkowe kata ya
Nkowe, wilayani Ruangwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
