Ngariba Tarime wapewa Elimu ya Ujasiriamali, ili kuacha kukeketa Msichana



Meneja
Miradi Shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga Vita Ukatili wa Kijinsia
Wilayani Tarime Mkoani Mara Valerian Mgani akifafanua jambo kwa Ngariba
na baadhi ya waliokuwa Ngariba lakini kwa sasa  wameacha Ukeketaji
baada ya kupatiwa Elimu katika Mafunzo ya Siku Mbili kuhusu madhara ya
Ukeketaji na suala la Ujasiriamali ili waweze kuondokana na kutegemea
pesa za Ukeketaji.

Ngariba hao wamedai kuwa katika kipindi cha
Tohara upata pesa nyingi zaidi ya Mill tatu na hicho ndo kilikuwa kipato
chao sasa kwa kuwa Serikali inapiga Vita suala hilo kwa kushirikiana na
Mashirika waone jinsi ya kuwasaidia ili kijikwamua Kiuchumi na siyo
kutegemea tena Ukeketaji.


Jemida Kulanga ambaye ni Mwezeshaji wa Semina hiyo ya Siku mbili katika ukumbi wa MCN Mjini Tarime akiendelea na Somo.

Mmoja
ya waliokuwa Ngariba kutoka Koo ya Butimbaru akifafanua jambo ambapo
amesema kuwa kuwa kwa sasa wao hawakeketi bali wanapaka unga Usoni kwa
lengo la kutimiza Mila zao.

                   ,,,Tazama Video kupata habari Kamili,,,
Powered by Blogger.