Wazee wa Mila 40 Tarime wapewa Elimu ya Ujasiriamali



Wazee
wa Mila 40 Muungano koo12 kabila la wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara
wakiwa katika Mafunzo ya Ujasiriamali ili kuondokana na suala la
kutegemea pesa zinazotokana na Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

Valerian
Mgani ambaye ni Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga amesemakuwa
Wazee wa Mila wamekuwa wakisimamia suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike
na kujipatia Kipato lakini sasa wameamua kuwapatia Mafunzo hayo na kisha
wataunda vikundi vya watu watano na kuwapatia Laki tano kila kikundi
kwa ajili ya kuanzia ili wasitegemee tena pesa za Ukeketaji.


Vikundi hivi vitasajiliwa na Halmashauri pia wazee hawa watatumia
vikundi hivi kukopa pesa kwa ajili ya kuendesha Miradi yao hata kama ni
Ufugaji,, Kilimo na Biashara ndogondogo alisema Valerian




     ,,,Tazama Video hapa Chini kupata habari Kamili,,,,
  
Powered by Blogger.