Makamu Wa Rais Apokea Vifaa Vya Upasuaji Kutoka Ubalozi Wa Kuwait
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema uboreshaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kama MOI,
zitaipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi na hivyo
kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha huduma za afya
kwa wananchi.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati wa kupokea vifaa vya Chumba Cha Upasuaji
wa Watoto vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa Taasisi ya Mifupa (MOI)
jana tarehe 15 Mei, 2018.
“
Aidha kwa namna ya kipekee nakushukuru Mheshimiwa Balozi wewe binafsi
na Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano ambao mnaendelea kuipatia Serikali
yetu ya awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali za maendeleo lakini hasa
hasa katika sekta ya afya” alishukuru Makamu wa Rais.
Makamu
wa Rais alisema kuwa Balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al Najem amekuwa
mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Afya hapa nchini ambapo leo
wamesaidia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 258 ambavyo
vitaiwezesha Taasisi kuimarisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa kwa
watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Makamu
wa Rais amlisema msaada huo utaiwezesha Taasisi kuwa na chumba cha
upasuaji ambacho kitakuwa maalum kwa watoto tu, hivyo idadi ya wagonjwa
watakaopata huduma ya upasuaji itaongezeka kutoka 500-700 kwa mwezi,
kufikia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa mwezi na watahudumiwa kwa haraka
zaidi.
Wakati
huo huo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Faustine Ndugulile amesema Tanzania iatendelea kuimarisha
uhusiano na nchi ya Kuwait kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa
msaada haswa msaada inayohusu sekta ya afya.
Balozi
wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem alisema kuwa Wananchi wa
Kuwait wana mapenzi makubwa na Watanzania na kuahidi wataendelea kutoa
msaada.
