Akutwa amefariki Mtoni Tarime

Mwili wa Marehemu ukiwa katika Maji ya Mto Nyabirundu Kijiji cha Nyabichune kata ya Regicheri Wilayani Tarime Mkoani Mara.
Na CLEO24NEWS TARIME.
Mtu Mmoja ambaye hajafaamika kwa Jina wala Sura amekutwa amefariki na Mwili wake ukiwa katika bonde la Mto Nyabirundu uliopo kitongoji cha Nyabichune Kijiji Nyabichune kata ya Regicheri Wilayani Tarime Makoani Mara.
Shuhuda wa kwanza katika tukio hilo amesema kuwa majira ya asbuhi jana alipoenda kuchimba Mchanga Maeneo hayo aliona Mwili huo wa Marehemu na kukimbia kutoa taarifa kwa Viongozi wa Vitongoji na vijiji.
Elias Mbusiro ni Mwenyekiti wa Kitongoji alichokutwa Marehemu huyo pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha NyabichuneFrancis Mwikwabe wakizungumzia tukio hilo wamesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walipiga simu kwa viongozi ngazi za juu ili kufika eneo la tukio kwa lengo la kupatiwa Msaada.
“Huyu marehemu anaonekana Mzee lakini bado sura yake hatujaitambua katika kijiji chetu kama ni Mkazi wa hapa” alisema Mbusiro.
Meshaki Osward ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Regesheri amedhibitisha uwepo wa Tukio hilo huku akitoa Mwito kwa jamii kujitokeza ili kutambua Mwili huo.
“Polisi tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kuchukua Mwili huo kama sisi viongozi mpaka sasa hatujautambua Mwili huu, kama kuna mtu yeyote amepoteza Ndugu yake apige simu Polisi Sirari au Kwa Viongozi wa Vijiji na Kata tukio lililopotokea” alisema Meshaki.
Badhi ya Viongozi wa Vijiji na kata wakiwa katika Wneo la tukio