Wahamiaji Walowezi Watakiwa Kujiorodhesha Uhamiaji
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewataka wahamiaji walowezi kujiorodheshwa katika ofisi zao za uhamiaji wilaya.
Lengo
ni kwamba baada ya kufanya hivyo watapewa vibali vya ukaazi
vitavyowafanya kuishi nchini kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dar es Salaam, na Naibu wa Idara ya Uhamiaji
Mkoa wa Dar es Salaam, Petro Malima na kuwa zoezi la uandikishaji
wahamiaji walowezi ni la nchi nzima.
“Hivyo
kwa wahamiaji walowezi lazima wajiorodheshe kwa kuwa na picha tatu za
Paspoti zilizo katika wakati na wenye watoto wanatakiwa kuwa na picha
tatu hizo”, alisema.
Aliongeza
kwa wale wataofanya hivyo watatambulika na kuendelea kuishi nchini bila
kusumbuliwa kuhusu masuala ya uhamiaji na kutofautisha na wakimbizi na
wahamiaji haramu.
Malima
alisema wageni wote wanatakiwa kuitikia mwito huo wa Serikali pamoja na
wale ambao wanaishi nchini na kufanyakazi au biashara kinyume na
sheria za nchi wanatakiwa kufika katika ofisi za wilaya ili kuhalalisha
ukaazi na kupewa vibali vinavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi.
Alisema yeyote atakayejificha katika mchakato huo na baadaye kubainika anaishi kinyume cha cha sheria hatua kali zitachukuliwa.
Hatua hizo ni pamoja na kufukuzwa nchini mara moja au kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kukiuka sheria.
Aidha
Malima alisema kuna matapeli wamekuwa wakiwasumbua wageni wanaoingia
nchini kwa kudai wao ni askari au maofisa wa uhamiaji na wakiwa hawana
hata sare.
“Viongozi
wetu wanajitahidi kwa kila hali kuitangaza nchi yetu na kuvutia
wawekezaji sisi uhamiaji Dar es Salaam hatuwezi kukaa kimya na kuona hii
ni nia njema ya Serikali inaharibiwa na watu wachache wasiotakia mema
nchi yetu."