Upatikanaji wa dawa waongezeka na kufikia asilimia 95
Serikali
yasema upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya
vya hospitali umefikia asilimia 95 kutoka ilivyokuwa awali 80% huku
ikibainisha kuwa bei ya dawa kushuka kwa 40%.
Serikali
imesema utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara Fly Over
umefikia asilimia 70 ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka
huu.
Serikali
imesema kuanzia mwezi Juni au Julai mwaka huu itaanza ujenzi wa
barabara za juu (FlyOver) kwenye makutano ya barabara za Chang’ombe,
Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni na Tabata, ujenzi huo
utasaidia kuondoa changamoto ya foleni jijini Dar es Salaam.
Awamu
ya pili ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam
unatarajiwa kuanza mwaka huu, mradi huo utahusisha ujenzi wa barabara za
mwendokasi za Kilwa hadi Mbagala, na Uhuru hadi Gongo la Mboto.
Serikali imepanga kubadilisha mfumo wa masoko ya mazao mbalimbali kwa kuanzisha Soko la Kimataifa la Bidhaa za Kilimo.