Rais Magufuli mgeni rasmi misa ya kusimikwa Askofu mteule Jackson kuwa Askofu wa tano wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam
Rais
John Magufuli ni mgeni rasmi katika misa ya kusimikwa Jackson Sosthenes
kuwa askofu wa tano wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es
Salaam.
Misa
ya kumsimika Askofu mteule Sosthenes inafanyika asubuhi ya leo Februari
4,2018 ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jacob
Chimeledya.
Viongozi
kadhaa wa Serikali akiwemo Rais Magufuli na mkewe Janeth; Rais mstaafu
Benjamin Mkapa, wanasiasa na waumini wa kanisa hilo wamewasili katika
Kanisa la Mtakatifu Albano lililoko eneo la Posta jijini Dar es Salaam
inakofanyika misa hiyo.
Baadhi
ya viongozi waliopo kanisani ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali
Venance Mabeyo; Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba; Waziri wa
Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi; Kamishna wa Uhamiaji, Dk
Anna Makakala; na Waziri Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala
Bora), George Mkuchika.
Sosthenes
anasimikwa kuwa askofu kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk Valentino
Mokiwa aliyeondolewa madarakani na uongozi wa juu wa kanisa hilo
takriban mwaka mmoja uliopita.