MWANAUME ALIYEBEBA DAWA ZA KULEVYA KWENYE MAKALIO BANDIA AKAMATWA
Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanaume mmoja kwenye uwanja wa ndege
huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio
bandia.
Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil
aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil.
Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo.
Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo.
Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani
ya mananasi yaliyokuwa yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.
Chanzo- BBC
