JANGILI AUAWA KWA KULIWA NA SIMBA AKIWINDA WANYAMA
Moja ya habari kubwa wiki hii ni kuhusu
mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jangili katika hifadhi ya simba karibu na
Mbuga ya Wanyama ya Kruger amevamiwa na kuliwa na kikundi cha simba
akiwa katika shughuli zake hizo za uwindaji nchini Afrika Kusini.
Polisi katika eneo hilo wameeleza kuwa
mtu huyo ameraruriwa vibaya na vipande vichache tu vya mwili wake ndiyo
vimepatikana ikiwa ni pamoja na mabaki ya kichwa.
Wameeleza kuwa mpaka sasa haijajulikana mtu huyo ni nani lakini uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo wamegusia kuwa kumekuwa na
ujangili kwenye hifadhi hiyo, ambapo mwaka jana simba walipewa sumu na
kufa huku vichwa na kwato zao zikachukuliwa.