Mwanamke aungua moto Vikali baada ya kwenda kwa Mganga wa jadi Rorya



Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya SACP Henry Mwaibambe akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Watuhumiwa wawili ambao ni waganga
wa jadi wanaoshikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuunguza Mwanamke
Mmoja jina limeifadhiwa Mkazi wa kitongoji cha Ombasa Kijiji Omuga
Wilayani Rorya Mkoani Mara kwa madai wanatibu suala la kushindwa kupata
ujauzito.


Kamanda
amesema kuwa  Jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kumjeruhi mwanamke huyo watu hao ni Juma Ayoub Mkazi wa kijiji cha
Rabuor na Michael Jacob Mkazi wa Shirati ni baada ya mama huyo kutopata
ujauzito na ndipo aliamua kwenda kwa waganga na kupewa Mashariti kuwa
watamwagia kuku mafuta ya taa na alipomwagiwa mafuta hayo kuku
yalisambaa mikononi na kifuani mwa mwanamke huyo na walipowasha moto
mama akaanza kuungua vikali na kusababishiwa majeraha makali.


Kamanda akizungumzia tukio hilo.
 

Picha
za Mama jina limeifadhiwa   Mkazi wa kitongoji cha Ombasa Kijiji cha
Omuga Wilayani Rorya akiwa amelazwa katika hospitali ya Kowaki kwa
ajili ya Matibabu kutokana na kisa hicho kilitokea baada ya mama huyo kukosa kupata
ujauzito kwa muda mrefu nakuamua kwenda kwa waganga nakupewa k mashariti hayo ambayo yamesababisha
maumivu Makali.


         Tazama Video Mganga wa jadi akizungumzia suala hilo, Kamanda alaani vikali kitendo hicho.
Powered by Blogger.