Magufuli ambadilikia Waziri na Mwanasheria Mkuu
Rais
Dkt. Magufuli leo Februari 1, 2018 amewabadilikia Waziri wa Katiba na
Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali, George
Masaju kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia
kazi mambo ya msingi.
Magufuli
amesema hayo alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria na kusema
yeye ameubwa kusema ukweli hivyo ataendelea kuusema hata kama kuna watu
unawaumiza
"Kinachoshangaza
pamoja na hatua nzuri ya Serikali kupeleka 'Legal Aid Act' ya mwaka
2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini
'regulation' mpaka saizi hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria,
tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo
"Jamani
mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa, kwa hiyo wewe
Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna 'Instrument' za kuweza kutoa
uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini
regulations mpaka leo miezi tisa imepita.
"Watu
wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi
wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi
haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania.
"
Ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo ndani ya Serikali lazima
na mimi nijitathimini ninachaguaagaje hawa watu ambao wanachelewesha
chelewesha, hiyo ndiyo tathimini ambayo ninaanza kujifanyia kuanzia leo"
alisema Rais Magufuli