Kampuni ya simu TTCL yabadilishwa Rasmi
Serikali
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo Februari 1, 2018 imefanya
mabadiliko na kuibadili kampuni ya simu ya TTCL kuwa shirika la Umma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametangaza
maamuz hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa
mabadiliko hayo hayawezi kuathiri wateja wa TTCL
"Sasa
tunatoka kwenye TTCL kampuni na kuwa shirika la Umma tunaamini saizi
mtajipanga zaidi kwenye mambo ya usalama na uimarishaji mambo ya uchumi.
Pia napenda kuwajulisha Watanzania kuwa mabadiliko haya hayatawaathiri
kwa namna ya utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zilikuwa zikitolewa na
kampuni ya simu ya TTCL, huduma zote zilizokuwa zikitolewa kuanzia
kwenye simu za mkononi, data, enternet, TTCL Pesa zote zitaendelea sasa
kwa kiwango kikubwa zaidi" alisema Mbarawa
Mbali
na hilo Mbarawa amewataka TTCL sasa kufanya jitihada za kwenda
kukusanya madeni yake kwa wananchi mbalimbali ambao wanatumia huduma zao
na kusema kuwa Serikali inatambua ina deni kwa TTCL na kuwa wao
watalipa na wako tayari kulipa ila wanapaswa kuanza kwenda kudai fedha
zao kwa wananchi mbalimbali na makampuni ambayo pia yanadaiwa na TTCL.