Waziri Lukuvi atangaza uamuzi mzito Mwanza
WANANCHI wanaomiliki nyumba 664 katika
mitaa ya Kigoto na Kabuhoro katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela
jijini Mwanza wametakiwa kuwa na subira wakati serikali ikitafuta
ufumbuzi wa mgogoro uliopo kati yao na Jeshi la Polisi.
Pia
wamezuiwa kujenga nyumba zingine mpya kwenye maeneo ya mitaa yao na
badala yake wawe walinzi na kuonya watakaothubutu kujenga hawatalipwa
fidia ambapo awali walitakiwa kuondoka na kupisha eneo hilo baada ya
kuandikiwa ilani ya siku saba na jeshi la polisi.
Akizungumza
na wananchi hao Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William
Lukuvi alisema serikali imesikia kilio chao na hivyo amekuja chunguza
mgogoro huo ili ifanye uamuzi wa kuutatua.
Alisema
serikali inataka kufahamu mahitaji ya wananchi na polisi na kuonya
wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo wasithubutu kujenga (kuongeza)
majengo mengine zaidi ya yaliyopo sasa na watakaokaidi hawatalipwa
fidia.
“Nimekuja
kuangalia mgogoro huu na kuchungumza jambo hili ili serikali ifanye
uamuzi. Msidhani nina majibu, majibu yatatolewa ndani ya mwaka mmoja
lakini msituhubutu kuongeza nyumba zingine zaidi, kuweni walinzi wa
maeneo haya na tunataka muwe maeneo mzuri ili tuwarasimishie,”alisema
Lukuvi.
Waziri
huyo wa ardhi alisisitiza baada ya uchunguzi atamshauri vizuri Rais
John Magufuli namna ya kumaliza mgogoro huo baina ya wananchi na taasisi
hiyo ya serikali.
Lukuvi
alieleza eneo la Kigoto ambalo Polisi inadai inataka kujenga Chuo cha
Polisi wanamaji, nyumba za askari na gati la boti na meli za doria
zinaweza kujengwa popote lakini eneo hilo lazima lipangwe upya hata kama
matumizi yakibadilishwa kwa kuwa haiwezekani watu waishi kwenye nyumba
za ovyo ovyo.
“Miaka
70 hadi leo kwa nini ujenzi haukuzuiwa,hakuna viongozi hapa na kama
mngewashirikisha wangewasaidia kuzuia.Je, upembuzi yakinifu ulifanyika
kwenye eneo mnalotaka kujenga mdomo huo wa gati la boti za polisi?
Aidha
akizungumza kwa niaba ya wenzao ,Ferdinand Mtundubalo alimweleza Waziri
kuwa hawana tatizo na ujenzi wa gati la boti za polisi isipokuwa
warasimishiwe makazi yao ili waondokanane na mgogoro huo.
Katika
hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwataka wataalamu wa wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilemela waainishe eneo la Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Ihale ili kila mmoja alinde
eneo lake.
Pia
alishauri eneo la Nyamwilolelwa litakalobaki baada ya kutengwa la
uwanja wa ndege na JWTZ lipimwe wapewe wananchi wa eneo wapatao 1,961 na
kuhusu barabara ya Mwanza –Igombe uamuzi wa Rais Magufuli ubaki ulivyo
na uheshimiwe.