WAKULIMA WATUMIA SABUNI YA UNGA NA MCHANGA KUKABILIANA NA WADUDU WAHARIBIFU WA MAZAO.
Jacksoni Masunga mkulima wa Mahindi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mazao kushambuliwa na wadudu. |
Malimi Wilson Mkulima wa pamba wilayani Bariadi Mkoani Simiyu akizungumzia juu ya zao hilo kushambuliwa na wadudu.
Na COSTANTINE MATHIAS, SIMIYU.
WAKULIMA wa Mazao ya chakula na Biashara Wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamebuni mbinu mbadala ya kukabiliana na wadudu wanaoshambulia mazao yao baada ya wataalamu wa kilimo kutowasaidia.
Wakulima hao ambao kwa sasa wanatumia sabuni ya unga (foma) na mchanga ili kuuwa wadudu hao, wameitaka serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo kuhakikisha wananusuru hali hiyo.
Wakiongea wa waandishi wa habari waliowatembelea mshambani mwao walisema kuwa pamoja na seriklai kuwasisitiza kulima kwa wingi, lakini hakuna jitihada zozote wala hakuna wataalamu wa kilimo waliofika kuwatembelea mashambani. ‘’mazao yameliwa na wadudu, tumekosa dawa, hakuna wataalamu waliofika kututembela wala kukagua mazao yetu…wataalamu wamekaa ofisi badala ya kututemblea mashambani, tunatumia dawa za kienyeji ikiwemo kumwaga mchanga na sabuni ya unga’’ alisema Jacksoni Masunga mkazi wa Somanda.
Jackosi aliongeza kuwa wanaloweka sabuni ya unga kwenye maji na kuwapulizia wadudu katika mazao ya mahindi na pamba, lakini hawajapata suluhisho huku wakisisitiza mchanga kuwasaidia.
Tabitha Ngunda na Malimi Wilson ambao ni wakulima walisema kuwa kwa sasa mashamba yanashambuliwa na wa wadudu na hakuna jitihada zozote zinazofanywa na serikali. ‘’serikali imetuhamasisha kulima kwa wingi, lakini kwa sasa dawa hatuapati hata zilizoko madukani zinauzwa bei ghali na haziuwi wadudu, tumeona mbadala tutumie hizi za kienyeji’’ alisema Malimi.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoani Simiyu (UVCCM) umeitaka Serikali na Bodi ya Pamba nchini kuhakikisha wanatatua changamoto ya upungufu wa dawa za pamba unaowakabili wakulima.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani hapa Lumeni Mathias alisema kuwa Bodi ya Pamba isilifumbie macho suala hili, kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanaongeza kipato huku serikali nayo ikiongeza mapato, lakini kama zao hili likishambuliwa na wadudu watakuwa wamekwamisha adhma ya serikali ya Tanzania ya Viwanda. ‘’hatutanii wakulima wetu wa Pamba walihamasika sana, kama mazazo yao yanashambuliwa na wadudu bila udhibiti wowote, tutakuwa tumewavunja moyo na kuwaingiza kwenye hasara kubwa kutokana na gharama ambazo wameziingia katika kilimo’’ alisema Lumeni.
Aliongeza kuwa katika ziara waliyoifanya wamebaini vijiji vyenye wakulima wengi kupewa chupa chache za dawa, hali inayowafanya wakulima hao kushindwa namna ya kunusuru mazao yao. ‘’kijiji cha Ng’alita chenye vitongoji 10, na kila kitongoji chenye wakulia zaidi ya 400, kinapewa chupa 10…kijiji cha ipililo chenye wakulima 300 kinapewa chupa 50, kitongoji cha mwabakali chenye wakulima zaidi ya 200 kinapewa chupa 10…hili hatuwezi kulivulia lazima tuwasemee wakulima wetu’’ alisisitiza Lumeni.
Aidha wameitaka Bodi ya Pamba na Maafisa Ugani wa Wilaya na Mkoa kuhakikisha wanashughulikia mapema suala hilo kwa maslahi ya wakulima, huku wakifuatilia kwa haraka tatizo la viwavi jeshi vinavyoshambulia mazao ya wakulima hasa mahindi.
Busiga Mhandi ni Mkulima wa Kijiji cha Nyanguge wilayani Bariadi alisema kuwa tatizo la uhaba wa dawa ni la muda mrefu, serikali inatakiwa kulipatia ufumbuzi ili kuwanusuru wakulima hao.
Aliongeza kuwa serikali inatakiwa kusimamia ipasavyo juu ya upatikanaji wa dawa hizo ambazo badhi yake zimekuwa hazina ubora wala haziuwi, kuliko kujikita kukusanya ushuru wa pamba ambapo kipindi cha kilimo hawasimamii uzalishaji.