TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA MAJINA 27 YA WAGOMBEA UDIWANI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa
majina 27 ya wagombea udiwani walioteuliwa na wasimamizi wasaidizi wa
uchaguzi kuwania nafasi hizo katika kata 10.
Uchaguzi mdogo katika kata hizo utafanyika Februari 17,2018 kutokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu nyadhifa zao na vifo.
Katika uteuzi huo wanaume waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni 24 na wanawake ni watatu.
Taarifa iliyotolewa na NEC leo Ijumaa
Januari 26,2018 imesema wagombea wa kata nne waliteuliwa Januari 20 na
wengine wa kata sita waliteuliwa Januari 24,2018.
Wagombea waliojitokeza kuwania udiwani
katika kata ya Buhangaza iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera na vyama
vyao ni Jenitha Tibihenda (CCM), Nelson Makoti (Chadema) na Grayson
Aniceth (NCCR Mageuzi).
Katika Halmashauri ya Siha iliyoko
mkoani Kilimanjaro ambako kuna kata tatu zitakazofanya uchaguzi mdogo,
wagombea katika kata ya Gararagua ni Zakaria Lukumai (CCM) na Agness
Lasway (Chadema). Kata ya Donyomuruak wagombea ni Lwite Ndossi (CCM) na
Daniel Molle (Chadema), wakati katika kata ya Kashashi wagombea ni Suzan
Natai (CCM) na Immanuel Saro (Chadema).
Mkoani Mwanza ambako kuna kata mbili,
wagombea wa kata ya Kanbyelele iliyoko Halmashauri ya Misungwi ni Marco
Yela (ACT Wazalendo), Daniel Makoye (CCM) na George Mhoja (Chadema).
Kata ya Isamilo iliyoko wilayani Nyamagana wagombea ni Nyamasiriri Marwa
(CCM), John Kisyeri (Chadema), Hashim Ramadhan (CUF), Georgina
Kibendegele (DP) na Ramadhani Mtoro (UDP).
Kwenye kata ya Mitunguruni iliyoko
wilayani Singida wagombea ni Abdallah Mkoko (CCM), Manase Kijanga
(Chadema) na Abdallah Kinga (CUF).
Wagombea wa Kata ya Madanga iliyoko
wilayani Pangani mkoani Tanga ni Mohamed Abdallah (ACT Wazalendo),
Athuman Tunutu (CCM) na Swaibu Mwanyoka (CUF).
Mkoani Dodoma ambako pia kata mbili
zitafanya uchaguzi, kata ya Manzase iliyoko wilayani Chamwino wagombea
ni Amos Mloha (CCM), Alex Chalo (Chadema) na Ndahani Mazengo (Chaumma),
wakati kata ya Kimagai wilayani Mpwapwa mgombea ni Noah Lemto aliyepita
bila kupingwa.