SHINDANO LA UREMBO WA NGAMIA LAINGIA DOSARI
Ngamia
12 wamepoteza sifa za mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya
wamiliki wao kuwachoma sindano ya kubadili maumbile.
Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na
kushindanishwa kwa muonekano wa nyuso zao, nundu na maumbile yao.
Lakini majaji waliingia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya
udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za
fedha.Shindano lina vigezo vikali vya urembo
Vile vile tamasha hilo lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim dola milioni 57.
Mtandao wa habari wa The National imeripoti kuwa Ali Al Mazrouei, mwana
wa mfugaji bingwa , alisema dawa ya botox ilitumika kwenye midomo, pua
na hata taya.
"Dawa hiyo inavimbisha kichwa kwa hio ukimuona ngamia unadhani ana kichwa,mdomo na pua kubwa" aliezea Mazrouei.Tamasha hilo linasherekea tamaduni za Kisaudia
Majaji pia walikuwa wakishindanisha nundu na misuli ya ngamia.
Kabla ya tamasha hilo, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti daktari
wa wanyama alikamatwa akiwa pasua ngamia hao ili kuwabadilisha ukubwa wa
masikio pamoja na kuwachoma sindano ya dawa ya kubadilisha maumbile.
Jaji mkuu Fawzan al-Madi amesema kuwa ngamia ni moja wapo wa "nembo ya Saudi Arabi"
Mashindano hayo ya urembo wa ngamia yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2000.
Chanzo -BBC