PROF.SOSPETER MUHONGO AKABIDHI MILIONI 26 ZA MFUKO WA JIMBO AZIELEKEZA SEKTA YA ELIMU.


Picha ya pamoja wazee walioshiriki kikao cha kuunda baraza la wa zee Musoma Vijijini katikati ni Mbunge wa jimbo hilo Prof Sospeter Muhongo(aliye vaa koti nyeusi)


Prof . Muhongo Mbunge pili kutoka kushoto akiwa na wazee kutoka kata ya Musanja .


Prf. Muhongo akisamiliana na wazee kutoka kata ya Bugoji mara baada ya kikao hicho.


Prf.Muhongo Akifanya mazungumzao na baadhi ya wazeeejimbo la Musoma vijijini.






Na Makalinews. MARA.
Sospeter Muhongo amekabidhi fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi milioni 26 ambazo hutolewa na serikali kupitia mfuko wa mbunge huku fedha zikielekezwa kwenye maendeleo ya jimbo hilo.

Prof. muhongo alielekeza  fedha hizo  idara ya elimu ili kukamilisha kuezeka maboma 15 ya vyumba vya madarasa katika jimbo hilo.

Mbunge huyo amelekeza  fedha za mfuko wa jimbo kwenye elimu pamoja na kilimo ikiwa nikipa umbele chake katika jimbo la musoma vijijini.
Mbunge huyo amekuwa akitoa kipaumbele kwa wananchi wake hususani kuwashirikisha katika ugawaji wa matumizi ya fedha hizo nijinsi gani zitatumika.

Pia prof.muhongo aliiagiza halmashauri kufatilia vifaa ambavyo vilitolewa na mbunge kama vinafanya kazi.

"Kamati ya mfuko wa jimbo fatilieni vifaa hivyo ikiwemo zile mashine za umwagiliaji tulizotoa kwenye vikundi vya vijana na akina mama kama zinafanya kazi vizuri na ambazo havifanyi kazi zichukuliwe wapewe watu ambao wako tayari kuzifanyia kazi maana zingine ziko halmashauri mpaka sasa hazijachukuliwa ”alisema Prf.muhongo .


Sambamba na hilo  aliwasihi umoja wa vijana  ccm pamoja na wazee wajimbo hilo kutumia fursa ya kuuda vikundi vitakavyo wawezesha kufungua miradi kupitia mfuko wa jimbo.


Wakati huo huo Wazee katika kata zote 21 za halmashauri ya Musoma Vijijini mkoani Mara wameanza kuunda mabaraza ya wazee katika kila kata na kijiji lengo ikiwa ni kuboresha huduma za kijamii pamoja na kurekebisha maadili ya vijana pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili kupitia vikao mbalimbali vya mabaraza hayo.

Wazee hao walisema  baadhi ya watu  katika jamii huwadharau hasa kwenye  huduma bora za kijamii ikiwa ni pamoja na huduma za afya, wamekuwa wakikoswa sehemu ya kujadili changamoto wanazokumbana nazo na kudai kuwa kupitia mabaraza hayo sasa kutarudisha heshima ya wazee katika jamii .

Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo mbele ya mbunge wa jimbo la musoma vijijini Professa Sospiter Muhongo pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo katika kijiji cha murangi wazee hao wamesema kutokana na kuporomoka kwa maadili hususani kwa vijana kumepelekea vijana kuwadharau wazee na hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo.

Mmoja wa wazee, akiwemo Mzee.Zakaria machebe akihojiwa na Makalinews mara baada ya kikao hicho alisema umoja huo utasaidia jamii kwa asilimia kubwa kuwepo kwa maadili na kurudisha mila zilizopuuzwa na vijana kwa madai ya utandawazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Musoma vijijini Charles Magoma alisema kutokana na kuporomoka kwa maadili  imepelekea baadhi ya vijana  kukwamisha shughuli za maendeleo katika vikao na mikutano mbalimbali ambapo amesema mabaraza ya wazee yatasaidia kurekebisha tabia.

Akizungumza katika kikao hicho mkurugenzi wa halmashauri ya musoma vijijini Bi.Frola Yongoro alisema kuwepo kwa baraza la wazee kwa kila kata itarahisisha  upatikanaji wa misaada mbalimbali kutoka serikalini ikiwemo huduma za kia afya (Bima za wazee)  na kijamii (misaada kwa wazee wasiojiweza ) aliwasihi wazee kupitia mabaraza yatakayoundwa yaweze kusimamia maendeleo na maadili katika kata zao.
Powered by Blogger.