News Alert : NECTA IMETANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017..YATAZAME HAPA
BOFYA <<HAPA>> KUONA MATOKEO YOTE KWA URAHISI KABISA
Baraza
la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo
ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Shule iliyoshika namba moja
inatoka Mbeya.
Jumla
ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne
mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu
ambapo wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985
sawa na asilimia 79.06.
Akitangaza
matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles
Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa
na asilimia 70.09.
Amesema
matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo
mwaka huu.
"Watahiniwa
77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya
mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.
Dk
Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika
mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi
katika karatasi yake ya majibu.