Meneja TBA Kigoma akamatw

Jeshi la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma.

Meneja huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.

Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika

Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.
Powered by Blogger.