Waziri Kalemani Awapo ONYO Watumishi TANESCO
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewatangazia kiama wafanyakazi wa
TANESCO nchini watakaoshirikiana na watu kuiba miundo mbinu ya umeme,
ili kuhakikisha huduma hiyo haihujumiwi kama zingine.
Dkt.
Kalemani ameyasema hayo jana alipokuwa akiongea na maafisa wa TANESCO,
na kusema shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa kufuatia umeme
unaopotea, kutokana na kuhujumiwa miundo mbinu yake, na wizi wa umeme
uliokithiri unaofanywa na baadhi ya wateja.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya TANESCO
kugundua wateja zaidi ya mia moja wanatumia umeme bila kulipia hali
inayolitia hasara shirika, baada ya kufanya operesheni maalum ya kukagua
watu wanaoiba umeme jijini Dar es salaam.
Kufuatia
operesheni hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakiyakimbia makazi yao
kuogopa kutiwa mikononi mwa polisi, na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria.