MBUNGE MATIKO ATUNUKIWA CHETI CHA KUTHAMINI MCHANGO WAKE WA KULIWEZESHA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA KIPOLISI TARIME-RORYA.
Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini CHADEMA Esther Matiko akionyesha cheti alichotunukiwa katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Kirimanjaro na kufunguliwa na makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan. |
Mbunge Matiko akikabidhiwa cheti hicho na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba. Pia Mwigulu amempongeza Mbunge huyo alivyoshirikiana na jeshi la polisi bila kujali itikadi za chama kwani yeye anatoka chama cha upinzani na maendeleo hayana chama wala itikadi na kuomba wananchi kutii sheria ya usalama barabarani ili kuokoa maisha yao maana jamii inataka kuishi. |
Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Tarime Rorya Jeseph Bukombe akiwa katika jengo hilo ambalo Mbunge amechangia kwa asilimia 40%pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, Bodaboda na Jeshi la Polisi.
IGP Sirro alipokuwa akizundua jengo hilo Wilayani Tarime Mkoani Mara. |
Baadhi ya wadau waliochangia jengo hilo |
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani SP Joseph Bukombe akisoma Hotuba kwa IGP Sirro katika ufunguzi wa Jengo hilo. |
Mbunge akionyesha cheti alichotunukiwa kwa kutambua mchango wake katika jeshi la polisi kikosi cha usalama Barabarani. |
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther Matiko (Chadema) akipokea Cheti cha kutambua mchango wake kwa Jeshi la Polisi kwa kusaidia Maendeleo ya Jeshi hilo hasa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya katika hafla ya ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika kitaifa Mkoani Kilimanjaro.
Miongoni mwa michango ya Mhe. Matiko kwa Jeshi hilo ni kujenga jengo la ofisi kwa ajili ya Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo kwa 40% linalotumiwa na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa.
Ikumbukwe lengo kubwa la Mhe Matiko kushiriki katika ujenzi wa Jengo hilo ni kusogeza huduma za Traffic Wilayani Tarime kutoka Wilayani Musoma ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa Leseni ya Udereva ambapo hivi sasa Mkoa mzima wa Mara utolewa Msoma tu.
IGP Simon Sirro alipokuja Wilayani Tarime katika ufunguzi wa Jengo hilo alipata taarifa ya Mchango wa Mhe Matiko na kuelezwa na Katibu wa Mbunge (Peter Magwi Michael) lengo kubwa la Mhe Matiko kuchangia ujenzi huo ni ili kuwawezesha Wananchi wa Tarime kupata Leseni ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na IGP Simon Sirro kuahidi Mtambo huo utakuja.
Naye Kamishima Mwandamizi wa Polisi SACP Fortunatus Muslim amemwakikishia Mhe Matiko kwa kuwa Jengo hilo limeshakamilika kwa Mchango wake na baadhi ya Wadau wakiwemo Bodaboda wa Tarime Mtambo huo utafika na kuanza kuzalisha Leseni kwa kushirikiana na TRA Tarime-Rorya.
Naye RTO wa Tarime-Rorya SP Joseph Bukombe amepata kusema kwenye maadhimisho hayo na kumshukuru Mhe Matiko kwa mchango wake mkubwa wa kujitoa kifedha na mawazo katika kuisaidia Ofisi yake.
Katika hafla hiyo ya Kilele cha Wiki ya nenda kwa usalama barabarani Vyeti hivyo vimetolewa kwa Taasisi mbalimbali zikiwemo Kampuni lakini kwa Mchango wa Mtu binafsi ni Mhe Matiko pekee aliyepata kutunukiwa Cheti hicho.
Tarime Yetu Mshikamano Kwa Wote
Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu
Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu
Imetolewa na
Peter Magwi Michael
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Tarime Mjini
Jimbo la Tarime Mjini