TCRA Yawaasa Wamiliki Wa Mitandao Ya Kijamii Kuchuja Habari Zao Kwa Weredi
Wamiliki
wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa
wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa
Redio ama televisheni za Mitandaoni.
Hayo
ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati
alipokutana wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa
habari.
Valerie
amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi
pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha jamii au mamlaka.
Amesema
kuwa takribani miaka mitano kulikuwa hakuna fursa za kupata matangazo
ya televisheni kupitia mitandao ya kijamii, lakini sasa imeenea kwa
watanzania wengi na inaendelea kuongezeka kadri ya teknolojia
inavyokuwa, hivyo kunahitajika kuwepo umuhimu wa kusimamia huduma ya
mitandao hiyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.
Valerie
amesema kuwa TCRA kupitia kamati ya maudhui inatambua na kuthamini
kuwepo kwa fursa ya upashanaji wa habari na serikali iliamua kuruhusu
huduma hiyo wakati miongozo na taratibu stahiki zikiendelea
kutayarishwa.
Amesema
vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii vya Radio, Televisheni na
bado teknolojia inaendelea kukua na haviwezi kuzuia kutokana na mfumo wa
upashanaji wa habari.
Mwenyekiti
huyo anasema habari zingine hazina tija kwa jamii na zingine zinaleta
uchochezi ndani ya jamii na wakati mwingine kuingilia faragha za watu
ambazo hazitakiwa kufikia jamii kama sehemu ya habari.
Amesema
wadau wa mitandao ya kijami na watumiaji wa mitandao hiyo wanahakikisha
wanahabarisha kwa kuzingatia habari zinazojenga umoja wa kitaifa,
mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu,
kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania.
Aidha
amesema habari za matusi katika mitandao ya kijamii hayavumiliki ,kwani
zinakiuka misingi ya uandishi na uhuru na wajibu wake.