RC Mara azindua rasmi maonyesho ya siku ya Mto Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr Charles Mlingwa akitembelea moja ya Banda katika Maonyesho ya Siku ya Mto Mara ambayo ufanyika kila Mwaka kwa kushirikisha Nchi Mbili Kenya na Tanzania kwa lengo la kutunza Mazingira ukiwemo Mto Mara ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika Tanzania Wilayani Tarime Mkoani Mara kauli mbiu inasema kuwa Afya ya Mto Mara kwa Maendeleo Endelevu. |
Kiongozi kutoka Nchini Kenya akionesha Mipaka na utunzaji wa Mazingira kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr Charles Mlingwa baada ya kutembelea banda hilo. |
Mkurugenzi wa kampuni ya Mara Online Mugini Jacob akieleza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dr Charles Mlingwa jinsi kampuni inavyofanya kazi |
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akikagua jiko baada ya kutembelea moja ya banda katika Maonyesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu TTC Tarime. |
Mkuu wa Mkoa wa Mara alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara Isack Kabugu alipotembelea banda la Mara Online katika Maonyesho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiongea na Wananchi katika maadhimisho hayo. |