RAIS MAGUFULI AVUNJA MAMLAKA YA UENDELEZAJI WA MJI WA KIGAMBONI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amevunja
Mamlaka ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo Septemba
13, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa amethibitisha hilo na
kusema kuwa Rais Magufuli ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa
Kigamboni na kuamua kuivunja mamlaka hiyo ya Uendelezaji wa Mji wa
Kigamboni (KDA).
"Usikivu ni sehemu ya utatuzi hatimaye Rais wa Jamhuli ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli aridhia uvunjwaji wa Mamlaka ya
uendelezaji wa mji wa Kigamboni (KDA). Akizungumza Waziri wa Ardhi Mhe.
Lukuvi leo katika ukumbi wa chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
amesema "Mhe. Rais ameniagiza niwaalifu kuwa leo amevunja rasmi KDA,
Ahsante Mhe. Rais kwa kutusikiliza" alisema Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni
Mgandilwa
Mwezi Juni, mwaka huu Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile
aliiomba serikali kukabidhi majukumu yote, yaliyokuwa yakifanywa na KDA
kwa Halmashauri ya Manispaa hiyo ili kuyatekeleza na kuendeleza mji mpya
wa Kigamboni.