MWINGINE APIGWA RISASI DAR NA WATU WASIOJULIKANA
Ikiwa ni siku tano tu zimepita tangu
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma, tukio lingine kama
hilo limetokea Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi
wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali Vincent Mritaba.
Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali
Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na
watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.
Hadi usiku wa jana Madaktari walikuwa wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine.