MTOTO MWENYE UALBINO AUAWA KWA KUNYOFOLEWA UBONGO
Mvulana wa umri wa miaka 17 ambaye ana ulemavu wa ngozi amepatikana akiwa ameuawa na ubongo wake kutolewa nchini Msumbiji.
Mkazi wa eneo la Tete, magharibi mwa Msumbiji, ambaye hakutaka jina lake
litajwe, amesema wazazi wa mvulana huyo walianza kumtafuta alipokosa
kurejea nyumbani.
Mwili wake ulipatikana ukiwa hauna mikono na miguu.
Aidha, kichwa chake kilikuwa kimepasuliwa na ubongo wake kutolewa.
Msemaji wa polisi wa mkoa wa Tete Lurdes Ferreira amesema polisi wataanzisha uchunguzi eneo ambalo uhalifu huo ulitokea.
Kisa hicho ndicho cha karibuni zaidi dhidi ya watu wenye ulemavu wa
ngozi ambao mara kwa mara hushambulia kwa sababu ya viungo vyao ambavyo
hudaiwa kutumiwa katika ushirikina.
Chanzo-BBC