KANISA LA ABC LASIMIKA WACHUNGAJI WAKE NA KUWEKA WAKFU KWA WAANGALIZI
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila,
akitoa mahubiri katika ibada maalumu ya kuwasimika wachungaji watano
na kuwawekea wakfu wengine watano kuwa waangalizi wa kanisa hilo katika
ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwasalimia
waumini wa kanisa hilo. Mchungaji Agbeja aliongoza ibada hiyo. Kulia ni
Mtumishi wa Mungu, Zephaniah Andrew Nyambele ambaye alikuwa ni
Mkalimali katika ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Asumpter Mshama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo akizungumza kwa niaba ya serikali.
Wachungaji
waliosimikwa. Kutoka kushoto ni Ezekiel Katani kutoka Mbeya, Mbarikiwa
Mwakatika kutoka Morogoro na Leonard Mandia, Cosmas Nchimbi Morogoro
na Joel Nsalila kutoka Dar es Salaam.
Wachungaji
waliowekwa wakfu kuwa waangalizi wa kanisa hilo katika majimbo. Kutoka
kushoto ni Prince Twahir Rubeya, George Ntara,, John Muhembano, Lois
Malali na Nathaniel Ndabila kutoka Mbeya na wengine waliobaki wanatoka
Dar es Salaam.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
Kwaya ikiimba nyimbo za kusifu.
Maombi yakifanyika.
Ibada ikiendelea.
Picha zikichukuliwa.
Wachungaji wakisimikwa. Katikati kushoto ni Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwasimika
wachungaji hao. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila
Ibada ikiendelea.
Wachungaji hao wakisimikwa.
Ibada ya kuwasimika ikiendelea.
Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja akiwapaka
mafuta wachungaji hao.
Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja, akiwaombea
wachungaji hao wakati wa kuwasimika. Wa pili kushoto ni Mama Askofu
Rev. Flaston Ndabila na wachungaji wengine wakishiriki kuwaombea
wachungaji hao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila, akiwaombea wachungaji hao waliosimikwa.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC), Rev. Flaston Ndabila, akiwapongeza wachungaji hao.
Wachungaji wakiwekwa wakfu kuwa waangalizi wa kanisa hilo.
Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja, akimpaka
mafuta Mchungaji, Lois Malali kuwa mwangalizi wa kanisa hilo.
Wachungaji hao wakiombewa na wachungaji wenzao.
Maombi yakiendelea.
Maombi yakifanyika.
Wake wa wachungaji hao wakiwa katika maombi.
Wachungaji hao uso kwa uso na wake zao katika ibada hiyo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC),. Rev. Flaston Ndabila, akihubiri katika ibada hiyo.
Na Dotto Mwaibale
VIONGOZI wa
Dini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kuyaunganisha makundi yote
yaliyopo kwenye makanisa yao ili kuliletea taifa la Tanzania maendeleo
badala ya kuyagawa.
Ombi hilo
limetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Abundant Blessing Centre (ABC),
Rev. Flaston Ndabila wakati akihubiri katika ibada maalumu ya
kuwasimika wachungaji watano na kuwawekea wakufu wengine watano kuwa
waangalizi wa kanisa hilo katika ibada iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana.
“Kazi kubwa
mlionayo ninyi wachungaji mliosimikwa leo hii ni kwenda kuwatumikia
watanzania na makundi mengine yote yaliyopo katika makanisa yenu badala
ya kuyagawa” alisema Rev. Ndabila.
Rev.
Ndabila aliyataja makundi hayo yaliyopo makanisa kuwa ni wanasheria,
wataalamu, wanasiasa, wajane watoto na yale yenye uhitaji maalumu ambapo
aliwata wachungaji hao kwenda kuwatumikia na kuwaunganisha bila kujali
itikadi zao kwani kanisa halina ubaguzi.
Alisema
ndani ya makundi hayo wapo watu wanahitaji faraja hivyo waende wakawape
faraja badala ya kuwatenga kwani faraja watakayopata itawasaidia wasonga
mbele kiimani na kimaendeleo.
Alisema
Tanzania inataka kiongozi atakayekuwa anawaunganisha wananchi bila
kujali mtu huyo anatoka kundi gani na ana itikadi gani lengo likiwa ni
kuleta maendeleo ya nchi.
Aliongeza
kuwa kiongozi anayetakiwa ni yule atakaye saidia watanzania kupata
ufahamu wa kujua utajiri uliopo nchini na rasilimali zilizopo na jinsi
zitakavyo wanufaisha na kuondoa dhana ya kuwa nchi yetu ni maskini licha
ya kuwa ni tajiri.
Katika
hatua nyingine Askofu Ndabila aliwataka wananchi kujenga tabia ya
kuthamini juhudi mbalimbali za kuliletea taifa maendeleo zinazofanywa na
viongozi akiwemo Rais wetu Dk. John Magufuli ili kuwatia moyo badala ya
kuwabeza.
“Viongozi
wetu wanafanya juhudi mbalimbali za kuijenga nchi ni vizuri wote kwa
pamoja tukawatia moyo badala ya kuwabeza” alisema Ndabila.
Askofu
Ndabila aliwataka wachungaji hao kwenda kuwatumikia wananchi kupitia
kanisa badala ya kutumia madhabahu kwa ajili ya kujitajirisha na kuwa
wabinafsi ambapo pia aliwaonya kuacha kutumia lugha isiyoeleweka kwa
waumini wao badala yake watumie lugha nyepesi wanayoifahamu kama lugha
ya taifa jambo litakalosaidia kuondoa mikanganyo wanapotoa mahubiri.
Mwangalizi
wa Kimataifa wa Makanisa ya Christ Apostolic Church (CAC), kutoka
America ya Kaskazini, Mchungaji Dk.Timothy Omolayo Agbeja alisema
,Tanzania ni nchi ya amani na iliyojaa neema ambapo amewaomba watanzania
waendelee kuitunza.
“Nawaomba
watanzania tunzeni amani mliyonayo ,nimetembea nchi nyingi lakini
nimeona kuwa Tanzania ni moja ya nchi yenye amani watu katika makanisa
wana abudu kwa furaha kutokana na amani iliyopo hivyo hamna budi
kuitunza amani hii” alisema Dk. Omolayo.
Dk. Omolayo
alisema alishangaa watu wakiuza matunda mengi ambayo ni mazuri mitaani
tofauti na nchi nyingine hali ambayo inatokana na nchi iliyobarikiwa kwa
kuwa na ardhi yenye rutuba.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ibada hiyo kwa niaba ya serikali, Asumpter
Mshama aliwataka waumini wa dini zote wasiwe watu wa kutoa lawama kwa
serikali kuwa haifanyi chochote bali waisaidie serikali ili kuiletea
nchi maendeleo kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Dk.John
Magufuli.